Acts 3:2-7

2 aBasi palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa. Alichukuliwa na kuwekwa kwenye lango la Hekalu liitwalo Zuri, kila siku ili aombe msaada kwa watu wanaoingia Hekaluni. 3Huyu mtu alipowaona Petro na Yohana wakikaribia kuingia Hekaluni, akawaomba wampe sadaka. 4 bWakamkazia macho, kisha Petro akamwambia, “Tutazame sisi.” 5Hivyo yule mtu akawatazama, akitazamia kupata kitu kutoka kwao.

6 cNdipo Petro akamwambia, “Sina fedha wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Isa Al-Masihi wa Nasiri, tembea!” 7Petro akamshika yule mtu kwa mkono wa kuume akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikapata nguvu.
Copyright information for SwhKC